Nyimbo Mpya : Rayvanny, Guchi Waachia Video ya ‘Jennifer Remix’

[Picha: Guchi Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mtendaji wa Next Level Music Rayvanny hatimaye ameachia video ya Jennifer Remix ambayo alishirikiana na msanii wa Nigeria Guchi. Kutolewa kwa video hiyo kunakuja siku chache baada ya Guchi kutua Tanzania ambako anafanya miradi mingine kadhaa ya muziki.

Soma Pia: Msanii Guchi Kutokea Nigeria Azungumzia Kufananishwa na Zuchu

Video hiyo ilipokelewa vyema na mashabiki na ilipata takriban watazamaji elfu hamsini na tano ndani ya dakika hamsini na tano za kuchapishwa kwake.

Video ya ‘Jennifer Remix’ ilitengenezwa na lebo ya rekodi ya Next Level Music na hii ni kati ya nyimbo za kwanza kutoka kwa lebo hiyo mpya.

Rayvanny hapo awali alifunua kuwa atafanya kazi kwenye nyimbo zingine nyingi na msanii Guchi chini ya lebo yake ya rekodi.

Rayvanny akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege alipomkaribisha Guchi, aliweka wazi kuwa atamshirikisha Guchi katika miradi mingine, na kuongeza kwamba aliamua kufanya kazi na Guchi kwa sababu yeye ni mwanamuziki anayejituma na hutoa muziki mzuri.

"Mimi najua muziki mzuri na kila mtu anajua mziki mzuri. Wimbo huo nilikua naupenda sana lakini yeye mwenyewe pia baada ya kuongea naye akasema yes kwa sababu tunataka kufanya kazi nyingine akasema no, tuanze na remix ya Jeniffer kwanza," Rayvanny alisema.

 Kwa upande wake, Guchi alisema kuwa anapenda midundo za nyimbo za kibongo na amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na wanamuziki wa Kitanzania. Pia alisema kuwa mtindo wake wa muziki karibu unafanana na ule wa bongo.

https://www.youtube.com/watch?v=2bXXaiwh1Zg&ab_channel=Rayvanny

Leave your comment