Harmonize Ajibu Madai ya Kununua Watazamaji YouTube Kwenye Wimbo wake ‘Sandakalawe’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi Mtendaji wa Konde Music Worldwide Harmonize amejitokeza kujibu madai kwamba alinunua watazamaji kwenye wimbo wake wa hivi karibuni wa ‘Sandakalawe’.

Katika taarifa ambayo alichapisha kwenye mitandao ya kijamii, Harmonize alimjibu kwa kejeli mmoja wa mashabiki ambaye alikuwa amedai watazamaji kwenye wimbo wake walikuwa bandia.

Soma Pia: Maswali Yaibuka Kuhusu Idadi ya Watazamaji Kwenye Wimbo wake Harmonize 'Sandakalawe'

Harmonize alidai kuwa licha ya tuhuma kuwa watazamaji wa wimbo huo ni bandia, wimbo wake Sandakalawe bado ulikuwa unavuma na kuchezwa sehemu mbali mbali za ulimwengu.

Alisema kuwa watu walikuwa wakifurahiya wimbo wake licha ya mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

"Smash Them ISSA Party Everywhere," Harmonize aliandika.

Utata umeibuka baada ya wimbo huo kushindwa kuwa namba moja kwenye orodha ya video zinazovuma kwenye YouTube licha ya kupata idadi kubwa ya watazamaji.

Nyimbo zingine ambazo ziko kwenye orodha ya video zinazotamba zina watazamaji wachache kuliko wale wa Harmonize. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba YouTube hufanya ukaguzi wa watazamaji kabla ya kuidhinisha idadi hiyo kuonekana na umma.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

YouTube pia huadhibu yeyote ambaye atapatikana na hatia ya kununua watazamaji. Kwa hivyo, sio hatari tu, bali pia ni ngumu kwa mwanamuziki anayeheshimika kama vile Harmonize kununua watazamaji haswa kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwa Harmonize kukabiliwa na tuhuma kama hizo.

Leave your comment