Jokate Mwegelo Azungumzia Uteuzi wa Wasanii Katika Uongozi Nchini Tanzania

[Picha: Wikipedia]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Dar es Salaam Jokate Mwegelo amejitokeza kuelezea furaha yake kwa utambulisho wa wanamuziki na Rais Samia Suluhu katika serikali yake.

Jokate Mwegelo alisema kuwa utendajikazi mzuri miongoni mwa viongozi wa ujana ndio ulichochea serikali kutoa fursa zaidi kwa vijana haswa wasanii.

Jokate Mwegelo alikuwa akijibu swali juu ya maoni yake kuhusu uteuzi wa mwanamuziki wa Hip Hop Nikki Wa Pili kama mkuu wa Kisarawe. Alielezea kuwa ni jambo zuri kwa serikali kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha ujuzi wao wa uongozi.

Soma Pia: Weusi Waeleza Jinsi Kundi Lao Litabadilika Baada ya Nikki wa Pili Kufanywa Mkuu wa Wilaya

Jokate alielezea uaminifu aliyonayo katika uongozi wa Nikki Wa Pili na kuongeza kuwa alikuwa kiongozi mzuri ambaye amejitahidi kuendeleza Kisarawe.

Kulingana na Jokate Mwegelo, vijana pia wana mapungufu yao na hawapaswi kuhukumiwa kwa hilo. Alielezea kuwa ujana unaambatana na kufanya makosa.

"Sisi tulipoteuliwa watu wengi walikua na tafsiri tofauti, lakini kwa sababu tumeweza kuacha alama nzuri imeupa moyo uongozi wetu kuaminia watu wanaotoka katika tasnia mbali mbali mbali kuaminia kwamba na wao waneza kuwa na mchango chanya kwenye serikali yao," Jokate Mwegelo alisema.

Soma Pia: Nikki wa Pili Kubaki na Kikundi cha Weusi Licha ya Kuapishwa Mkuu wa Wilaya

"Kikubwa sisi vijana tuwe na ustaarabu na utaratibu wa wanafunzi, kukubali wengine, na unaweza kuona kuwa unakaribisha kujiuliza kuwa kuna sehemu sikufanya vizuri basi unaweza kurekebisha," Jokate aliongezea.

Aidha wasanii mbali mbali wamejitokeza na kumpongeza Nikki Wa Pili kwa uteuzi wake kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Leave your comment