Naibu Rais wa WCB Rommy Jones Amuagiza Diamond Kuachia Wimbo Mpya

[Picha: Romy Jones Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Makamu wa rais wa label ya WCB Rommy Jones ameamua kuvunja ukimya kwa kumuomba Diamond Platnumz atoe wimbo mpya. Rommy Jones ambaye ni binamu wa Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha picha yenye maneno yaliyosomeka: "Basi Diamond kama kaka ako na watanzania kwa ujumla tunakuomba utoe nyimbo."

Read Also: Maswali Yaibuka Baada ya Diamond Kuachia Kionjo cha Wimbo Wake Mpya

Ujumbe huo wa Rommy Jones ambaye pia ndiye DJ rasmi wa Diamond Platnumz unachagizwa na vilio vya mashabiki wengi wa Diamond Platnumz ambao kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakimsihi Diamond atoe wimbo maana ni miezi sita sasa imepita na hawajasikia chochote kutoka kwa msanii huyo.

Mara ya mwisho Diamond Platnumz kutoa wimbo ilikuwa ni November 30 mwaka 2020 na tangu hapo hajatoa ngoma yoyote bali alishiriki katika wimbo wa mbosso Baikoko pamoja wimbo wa Lavalava Far Away.

Kwa sasa, Diamond Platnumz yupo kwenye maandalizi ya albamu yake inayotarajiwa kuachiwa muda si mrefu na siku chache zilizopita alizua gumzo baada ya kupost video iliyodhaniwa ni kionjo cha wimbo wake mpya.

Soma Pia: Diamond Aeleza Mbona Hajaachia Wimbo Mpya Mwaka Huu

Rommy Jones ni Nani?

Rommy Jones ni binamu yake Diamond Platnumz, Rommy Jones akiwa amempita Diamond mwaka mmoja. Rommy huonekana akisafiri na Diamond Platnumz sehemu tofauti tofauti hasa kwenye matamasha ambapo Rommy Jones ndiye DJ rasmi wa Diamond Platnumz.

Kwenye muziki hutumia jina la Rj the Dj ambapo Julai mwaka jana alitoa album inayoitwa Changes akiwashirikisha wasanii kutokea Tanzania kama vile Lavalava, Rayvanny, Chin Bees, Christian Bella, Vanessa Mdee, Khadija Kopa, Mbosso, Marioo na Mimi Mars na nje ya Tanzania Ycee, Morgan Heritage, Jose Chameleone na Sho Madjozi walishiriki.

Leave your comment