Maswali Yaibuka Baada ya Diamond Kuachia Kionjo cha Wimbo Wake Mpya

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota nchini Tanzania Diamond Platnumz hivi karibuni alivutia watu kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha video fupi ya wimbo wake mpya uliopewa jina la "Loyal".

Soma Pia: Video ya Diamond Platnumz Kwenye Instagram Yazua Gumzo Mtandaoni

Katika video hiyo ambayo Diamond alichapisha kwenye mtandao, anaonekana akiimba akiwa pamoja na mwanamke fulani. Diamond katika wimbo huo anaelezea jinsi anavyompenda mchumba wake na anaahidi kuwa mwaminifu kwake.

Bosi wa WCB hakutoa habari zaidi juu ya wimbo huo na aliwaacha mashabiki wake wakiwa na hamu sana kujua ni kipi kilichoko kwenye wimbo huo mpya.

Video hiyo fupi sasa imeibua maswali kati ya watumiaji wa mitandao ya kijamii. Suala la kwanza ambalo limevutia mashabiki wengi ni iwapo Diamond atatumia wimbo huo kumtambulisha mpenzi wake. Diamond anajulikana kwa kuwaimbia wapenzi wake. Ana nyimbo kadhaa ambazo aliwaimbia wachumba wake wa zamani.

Soma Pia: Zuchu ‘Nyumba Ndogo’: New Music Tanzania [Official Dance Video]

Swali lingine ambalo pia limekuwa gumzo kati ya mashabiki wake ni kufanana kati ya wimbo wa Diamond na ule wa mwenzake wa Nigeria Wizkid 'Essence'. Baadhi ya wanamtandao wamesema kuwa nyimbo hizo mbili zinafanana sana na kuuliza iwapo Diamond anaweza kuwa amekopa wazo la wimbo huo kutoka kwa wimbo wa Wizkid.

Bado haijulikani wazi ikiwa Diamond atatoa wimbo moja au albamu.

Leave your comment