BET Yatangaza Kutokuwepo kwa Upigaji Kura Kwenye Tuzo za Mwaka Huu

[Picha: Archyde]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kampuni ya BET imejitokeza kutangaza kuwa hakutakuwa na upigaji kura katika toleo la kuwazawadi wasanii waliobobea mwaka huu.

Tangazo hilo lilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii kupitia BET Africa. Kulingana na taarifa hiyo, upigaji kura uliruhusiwa tu katika kitengo kipya cha Best International Act.

Soma Pia: Romy Jones Azungumzia Wanaomkashifu Diamond Kwa Kuteuliwa Kwenya Tuzo za BET

Upigaji kura kwa washiriki katika kitengo hicho, hata hivyo, ulimalizika tarehe 11 mwezi Juni. Hii ilikuwa kinyume na matarajio ya watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambao waliamini kuwa upigaji kura bado haujafunguliwa.

"There is no voting available except for the best new international category which closed on 11th of June,” ilisema taarifa kutoka BET Africa.

Tuzo za BET hapo awali ziliagiza watumiaji wa mitandao za kijamii kutumia sehemu ya maoni ya machapisho yao kupiga kura kwa wagombea wao wanaowapenda.

Katika kitengo cha Best International Act, waanamuziki watatu kutoka Afrika waliorodheswa. Wanamuziki hao ni kama vile; Diamond Platnumz, Burna Boy, na Wizkid.

Soma Pia: Diamond Azungumzia Kupigwa Vita Baada ya Uteuzi wake kwenye Tuzo za BET

Nchini Tanzania, Diamond Platnumz amepokea lawama na ukosoaji kwa kuteuliwa kwenye tuzo za BET. Sehemu ya Watanzania ilizindua ombi kwenye mitandao ya kijamii kutaka Diamond Platnumz aondolewe kwenye tuzo za BET. Ombi hilo hata hivyo halikufanikiwa.

Diamond amejitokeza kusema kuwa anaheshimu maoni ya kila mtu pamoja na wale wasiomuunga mkono.

Leave your comment