Romy Jones Azungumzia Wanaomkashifu Diamond Kwa Kuteuliwa Kwenya Tuzo za BET

[Picha: Romy Jones Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

DJ maarufu nchini Tanzania Romy Jones ambaye pia ni kaka wa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz amejibu shutuma dhidi ya Diamond Kufuata uteuzi wake kwenye tuzo za BET.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

Hivi karibuni, Diamond alilalamikiwa sana baada ya kutajwa kama mteule katika tuzo za BET kwa kitengo cha Best International Act. Kulingana na wale wanaomkosoa Diamond, mwimbaji huyo hastahili kuwa katika tuzo hizo za kifahari kwa sababu aliunga mkono serikali ya Rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli Pombe.

Akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, Romy Jones alimtetea Diamond Platnumz na kueleza kuwa kuwa watu hawawezi kulazimishwa kumpenda Diamond na wana haki ya maoni yao.

Soma Pia: Diamond Ashutumu Forbes kwa Kudharau Tasnia ya Muziki ya Tanzania

Romy Jones aliongeza kuwa Yesu Kristo hakupendwa na kila mtu na haiwezekani mtu kukosa ukosoaji. Alibainisha kuwa anamshukuru Mungu kwa mafanikio ya Diamond licha ya hisia tofauti kutoka kwa Watanzania.

“Huwezi kulazimisha watu wote wakupende. Kikubwa ni kushukuru Mungu na pia uendelee kufanya kazi. Huwezi kujua ni kwa nini hawa hawasupport…Kama pia Yesu walimkana…Hivyo tumshukuru Mungu na tuendelee kufanya kazi," Romy Jones aliiambia vyombo vya habari.

Diamond pia kwenye mahojiano ya hapo awali alielezea kuwa anaheshimu maoni ya wakosoaji wake.

Leave your comment