Diamond Aeleza Mbona Hajaachia Wimbo Mpya Mwaka Huu

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika nchini Tanzania Diamond Platnumz amezungumzia kuchukua mda mrefu kuachia wimbo mpya na albamu yake tarajiwa, akisema kuwa hana haraka ya kuachia kazi mpya.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Diamond alisema kuwa ni vizuri kutoa nyimbo chache zinazofanya vizuri kuliko kutoa ngoma nyingi ambazo hazipati matokeo bora.

"Sina haraka ya kutoa nyimbo. Ndio maana mwaka jana nlitoa nyimbo mbili na mauzo yake na rekodi zake zikakua kubwa. Mwaka huu hadi leo sijatoa wimbo," Diamond alieleza.

Soma Pia: Diamond Azungumzia Kupigwa Vita Baada ya Uteuzi wake kwenye Tuzo za BET

Alifunua zaidi kuwa amemaliza kufanya kazi kwenye albamu yake na yuko katika hatua za mwisho.

Wiki kadhaa zilizipita, Diamond alikuwa nchini Afrika Kusini pamoja na wandani wake kushughulikia albamu hiyo inayotarajiwa kwa hamu.

Diamond ambaye ni mmoja wa wanamuziki wakubwa barani Afrika amekuwa kimya kwa takriban miezi sita. Mashabiki wake walikuwa wakipata wasiwasi juu ya ukimya wake wa muda mrefu.

 Mwaka jana Diamond alitoa nyimbo mbili tu ambazo zilifanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube. Wimbo wake wa mwisho uliopewa jina la "Waah" aliyomshirikisha mwanamuziki wa Kongo Kofi Olimide ulipokelewa vyema na mashabiki na kupata watazamaji zaidi ya milioni sabini.

Wiki iliyopita, Diamond alifunua kupitia mitandao ya kijamii kuwa atatoa wimbo mpya hivi karibuni.

Leave your comment