Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

[Picha: CitiMuzik]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wa Bongo Fleva wanaendelea kuonyesha umahiri wao eneo la Afrika Mashariki kwa kuachia ngoma mpya zinazotamba.

Wasanii wengi tajika wameachia ngoma kadhaa mwaka huu, huku wengine wakitarajiwa kuachia nyimbo zao na albamu hivi karibuni.

Soma Pia: Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Katika nakala hii, tunaangazia wasanii wanaotarajiwa kuachia kazi mpya hivi karibuni:

Zuchu

Zuchu aliacha wimbo wake wa ‘Sukari’ mapema mwakani na ikapokelewa vizuri. Baada ya wimbo huo, aliachia ‘Kazi Iendelee’ ya kumsifia Rais Samia Suluhu na baadaye kuchapa collabo na msani Olakira kutoka Nigeria.  Kando na hizo, msanii Zuchu hajaachia kazi ingine mwaka huu. Inakisiwa kuwa msanii huyo ataachia wibo mpya hivi karibuni ile kuwaburudisha wafuasi wake.

Diamond

Tangu mwaka huu uanze, Diamond haajachia wimbo wowote wa kibanafsi. Msanii huyo amekuwa akshirikishwa kweye kazi mbali mbali na wasanii chini ya lebo yake ya Wasafi records. Diamond amekuwa akishughulikia albamu yake inayotarajiwa hivi karibuni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Zuchu, Rayvanny, Mbosso na Lava Lava Mwezi Mei 2021 [Video]

Alikiba

Mwaka huu, Alikiba ameshirikishwa kwenye collabo na wasanii kama vile Branaba, Otile Brown, na Darassa. Hata hivyo, miezi kadha imepita bila yeye kuachia wimbo wa kibinafsi. Inasemekena kuwa msanii huyo anashughulikia alabamu yake inayotarajiwa hivi karibuni.

Maua Sama

Ngoma yake ya mwisho ilikuwa ‘Wivu’ alioachia miezi nne iliyopita akimshirikisha Aslay. Kwenye mazungumzo ya hivi karibuni, Maua Sama amewaomba wafuasi wake kutulia and kusubiri kwani ataachia kazi mpya hivi karibuni.

Wasanii wengine wanaotarajiwa kuachia kazi mpya ni kama vile Harmonize, Darassa, Juma Jux na wengine wengi.

Bible Verses I DJ Mix 2021 I Football Predictions For Today I   Davido Latest Songs I Diamond Platnumz

Leave your comment