Wimbo ‘Sere’ wa Zuchu na Ola Kira Wafikisha Watazamaji Milioni Mbili

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutoka Tanzania Zuchu anasherehekea baada ya wimbowa ‘Sere’ aliachia pamoja  na mwanamuziki wa Nig

eria Ola Kira kupata watazamaji milioni mbili kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Watanzania Waanzisha Kampeni ya Kutaka Diamond Kuondolewa Kwenye Tuzo za BET

Wimbo huo uliachiwa takriban mwezi mmoja uliopita tarehe ya 23, mwezi wa Aprili.

'Sere' ilichapishwa kwenye akaunti ya YouTube ya Ola Kira ambayo ina wafuasi takriban 364,000. Wakati wa kuchapishwa kwa ripoti hii, wimbo huo pia ulikuwa umepata maoni zaidi ya 2,000.

Wimbo huo umetayarishwa na lebo ya rekodi ya U And I Music kwa kushirikiana na lebo ya rekodi ya WCB ambayo imemsaini Zuchu.

Soma Pia: Tamasha la Nandy Festival Lapata Mafanikio Makubwa Kigoma

Katika lebo ya WCB, wasanii wanapata mamilioni ya watazamaji kwenye nyimbo zao ndani ya siku chache, na labda wimbo huo ungeweza kufanya vizuri zaidi ikiwa ungechapishwa kwenye akaunti ya YouTube ya Zuchu.

Zuchu ana wafuasi milioni moja ambao wanachangia sana kufanikiwa kwa nyimbo zake. Wimbo huo umempa Ola Kira mafanikio kwenye YouTube.

 'Sere' imekuwa wimbo wa tano unaotazamwa zaidi na wafuasi was Ola Kira kwenye YouTube.

Ola Kira alipata umaarufu kwa wimbo wake wa 'In My Maserati' ambao umepata watazamaji milioni 32 hadi sasa.

Zuchu na Ola Kira walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo waliwashukuru mashabiki wao.

https://www.youtube.com/watch?v=wht8D5mekJ8

Leave your comment