Watanzania Waanzisha Kampeni ya Kutaka Diamond Kuondolewa Kwenye Tuzo za BET

[Picha: 247TVNEWS]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Uteuzi wa mwanamuziki nyota Diamond Platnumz kwenye Tuzo za BET katika kitengo cha Best International Act imeibua maoni tofauti kutoka kwa Watanzania.

Kikundi moja cha Watanzania kimejitokeza kutaka Diamond Platnumz aondolewe kwenye tuzo hizo kama kwa sababu ya kuunga mkono serikali ya hayati rais John pombe Magufuli.

Soma Pia: Mama Dangote Awaelimisha Watanzania Jinsi ya Kumpigia Kura Diamond Kwenye Tuzo za BET

Watanzania wameanzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii ambapo wanakusanya kura katika juhudi za kumfanya Diamond atupwe nje ya tuzo hizo za kifahari.

Kampeni hiyo hadi sasa imepata kura 10,101 huku lengo lake likiwa kufikisha kura 15,000.

Soma Pia: Diamond Platnumz Ateuliwa kwa Tuzo za BET 2021

Hata hivyo, sio watanzania wote wanaotaka Diamond kuondolewa kwenye BET, kuna baadhi ya wengine ambao wanajivunia kuingia kwa Diamond kwenye tuzo za BET.

Idadi nzuri ya watu mashuhuri wametoka kuelezea uungaji mkono wao kwa bosi wa WCB.

Baadhi ya wanamuziki mashuhuri wamewahimiza wafuasi wao kumpigia kura Diamond na kuhakikisha kuwa tuzo hiyo inakwenda Tanzania.

Mgawanyiko ambao umeshuhudiwa unaweza kuathiri nafasi za Diamond kushinda tuzo hizo. Ikiwa wale ambao wanapingana na Diamond wataendelea kuwa na msimamo huo huo, basi mwimbaji huyo anaweza kosa kura zote za Watanzania kama inavyotarajiwa.

Kampeni hiyo ilianza baada ya mwanasiasa mmoja mashuhuri wa Tanzania kujitokeza kumkosoa waziwazi Diamond kwa kuunga mkono serikali badala ya kusimama na haki. Diamond atawania tuzo hiyo dhidi ya wanamuziki wa Nigeria Wizkid na Burna Boy.

Leave your comment