Rose Muhando Vs Christina Shusho: Nani Msani Bora wa Nyimbo za Injili?

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mziki wa injili nchini Tanzania ni moja wapo ya fani iliyo na wasanii wengi wakubwa. Kwa miaka mingi, wasanii hao wamekua kigezo kikubwa katika kutubariki na mziki wao kupitia talanta zao . Kati ya wasanii hao ni waimbaji maarufu wa kike Rose Muhando na Christina Shusho. Hivyo katika kuendelea kuonyesha ujuzi wao wameendela kuachia kazi mpya miaka kadhaa baadaye.

Katika nakala hii, tunaangazia uwezo wao katika sanaa:

Uzoefu

Rose Muhando ni msanii amekua kwenye ulungi wa muziki kwa muda mrefu sasa. Licha ya kupata changamoto hivi karibuni, Rose alirudi kwenye sanaa kwa kishindo mwaka 2020. Kwa jumla, Rose Muhando ana uzoefu wa miaka kumi na misaba katika sanaa huku Shusho akishabikiwa kwa miaka kumi hivi.

Soma Pia: Nyimbo za Injili za Kiswahili Kwenye Mdundo (Pakua bila Malipo)

Tuzo

Rose Muhando anasifika kwa kupata tuzo nyingi haswa kutoka nchini Tanzania na Kenya. Mwaka 2005 Rose alishinda Tuzo ya msanii bora wa kike na Wimbo Bora zaidi katika Tuzo za Muziki Tanzania, 2008 akashinda Tuzo ya msanii Bora wa Injili wa kike Afrika katika Grove Awards za Kenya na Hatimaye mwaka 2009 alishinda tuzo ya msanii bora Injili(TBC). Shusho naye ana Tuzo zake ambazo mwaka 2011 na 2013 alishinda Tuzo za Groove huko Kenya kama msanii Bora wa Kike.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rose Muhando Aachia Video Mpya ‘Wanyamazishe’

Albamu

Rose Muhando kwa sasa yuko katika albamu yake ya tano tangu kuanza mziki huku Shusho akisifiwa kuwa na albamu tatu na EP moja.

Mashabiki kwenye Mitandao ya kijamii

Nchini Tanzania mashabiki kwenye mtandao wa kijamii haswa Instgaram huwa kigezo kikubwa kuonyesha umaarufu na ukubwa msanii ila kwa sasa ukweli unakua tata kwa ajili wasanii hawa wawili ni wa nyakati mbili tofauti. Rose Muhando ana mashabiki zaiki ya elfu hamsini kwenye mtandao wa Instagram na YouTube ana wafuasi zaidi ya laki mbili. Christina Shusho kwenye Instagram ana mashabiki zaidi ya laki saba na Youtube akiwa na subscribers zaidi ya laki tatu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya za Injili 2021 [Video]

Watazamanji Kwenye YouTube

Rose Muhando alifungua chanelli yake ya YouTube mwaka wa 2019 na kwa jumla ana watamazaji milioni 16,589,505. Kwengineko, Christina Shusho alifungua mtandao wake mwaka wa 2013 na ana watazamaji milioni 33,499,713.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Bora za Nyimbo za Injili

Leave your comment