Nyimbo Mpya: Rose Muhando Aachia Video Mpya ‘Wanyamazishe’

[Picha: Rose Muhando Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa mziki wa injili Rose Muhando ameachia video mpya kwa jina ‘Wanyamazishe’. Hii ni video yake ya pili kutoka albamu yake ‘Uko Wapi Yesu?’

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Katika wimbo huu, Rose anaangazia maisha yake wakati alipatwa na changamoto za maisha.

Anaelezea kuwa wakati huo alikua anauguza majeraha ya kimwili na kiroho. Katika kanda hii tunaona Rose akimlilia Mungu awanyamazishe maadui zake, wote waliomsema.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Hivyo, anasema wakati binadamu wako radhi kukashifu na kumsimanga binadamu mwingine, sio kazi yako kuwanyamazisha wale ambao wanakuwazia mabaya kwani yupo Mungu atakae wanyamazisha.

Soma Pia: Nyimbo za Injili za Kiswahili Kwenye Mdundo (Pakua bila Malipo)

“Kwa kuwa walitangaza msiba juu yangu, Wala hawakutaka ipone nafsi yangu, Wakafanya sherehe kupitia jina langu, Waliona fahari kutangaza mauti yangu,Wakachuma na pesa kupitia jina langu…” aliimba Rose Muhando.

Hivyo, katika wimbo huu Rose anaangazia uwezo wa Mungu kuinua mtu yeyote kutoka kwenye dhiki hadi kwa kheri yake ya maisha.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rose Muhando Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Simba’

‘Wanyamazishe’ ni Ombi la Rose Muhando kwa mwenyezi Mungu huku akionyesha vile wambea hutumia nguvu mingi kuona mmoja wao anaumia.

Miaka michache iliopita, Rose Muhando aliacha kufanya mziki kufuatia shida zilizompata. Msanii huyo alipatia changamoto mingi na wakati mmoja alionekana akiombewa na muhubiri wa Kenya Pastor Ng’ang’a.

Baadae, alipata kusaidiwa na rais Uhuru Kenyatta katika kushughulikia matibabu yake hadi kupona.

https://www.youtube.com/watch?v=wi_Bbsde7Pw

Leave your comment