Nyimbo Mpya: Sukari na Video Zingine Bora za Zuchu Zinazovuma Bongo

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani tajika kutoka Bongo Zuchu amepata umaarufu mkubwa sana barani Afrika mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa. Lebo ya Wasafi imefanya kazi mzuri kuhakikisha kuwa msanii huyo amepokewa vizuri na kwa kweli matokeo yamekuwa bora.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo zake tano bora mwaka mmoja baada ya yeye kuzinduliwa:

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Sukari

Sukari ni wimbo unaoangazi uzuri ulioko ndani ya mapenzi . Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya millioni thelathini na moja ndani ya miezi mitatu.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Kumi za Bongo Zilizoachiwa Mwezi Aprili 2021

Litawachoma

Katika wimbo huu, Zuchu amemshirikisha Diamond Platnumz. Hii ulikua moja wa nyimbo mbili zilizochiwa mara moja ndani ya wasafi. Litawachoma iliangazia chuki za watu kuhusu mapenzi yake Zuchu na mpenziwe. Kufikia sasa watazamaji kwenye mtandao wa YouTube ni zaidi ya milioni kumi na tano.

https://www.youtube.com/watch?v=g9spgkHS2bs

Soma Pia: Waah vs Attitude: Je ni Collabo Gani Bora ya Diamond ama Harmonize?

Nobody  

Kwenye Nobody, Zuchu amemshirikisha Joeboy. Huu ni wimbo wake wa kwanza kushirikiana na msanii wa kimataifa. Nobody ilimpa Zuchu fursa ya kuimba lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kufikia soko hilo la magharibi.

https://www.youtube.com/watch?v=04Roh3SDyN0

Nisamehe

Huu ni wimbo kutoka EP yake ya ‘I am Zuchu’ iliyopokelewa kwa ukubwa na mashabiki wa Tanzania. Huu ni wimbo unaongazia uchungu wa kumuona mpenzi wako wa zamani akiingia kwenye ndoa. Ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya millioni Kumi.

https://www.youtube.com/watch?v=-Ze28ZMQlH4

Cheche

Zuchu amemshirikisha kwenye Diamond Platnumz kwenye wimbo huu. ‘Cheche’ ni wimbo wenye mdundo wa kizomba na kitaliano ambao ulimpa Zuchu sifa hadi nchi za kimataifa kwa ufundi wake katika sanaa. ‘Cheche’ ni wimbo wa upendo na furaha. Kwa sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni ishirini.

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI

Leave your comment