Wasifu wa Mbosso , Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano

[Picha: Ralingo]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mbosso ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: Mbosso

Jina Halisi: Mbwana Yusuf Kirung

Tarehe ya kuzaliwa: 3rd October 1991(29 years)

Aina ya mziki: Bongo Fleva

Maisha ya mapema ya Mbosso yalikuwaje?

Mbosso alizaliwa katika kijiji cha Kibiti, Tanzania. Mamake ni Hadija Salom ambaye alikuwa mkulima na baba Yusuf Kirungi ambaye alifanya kazi kama dereva wa matatu. Mbosso alisoma hadi kidato cha nne na akaamua kuacha shule na kuwasihi wazazi wake wamuache aende kujaribu bahati yake jijini Dar es Salaam.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Mbosso alianzaje kazi yake ya muziki na lini?

Alipofika mjini, Mbosso alijitahidi kuishi mitaani kwani hakuwa na mahali pa kuishi. Baada ya muda, alikutana na mmoja wa msimamizi mkubwa wa wasanii Mkubwa Fella ambaye alimchukua kwenye mbawa zake .

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Baadaye, Fella alisaini Mbosso chini ya lebo Mkubwa na wanawe. Baada ya kutafakari jinsi ya kumshughulikia Mbosso kimuziki, alimuunganisha na kundi lingine la wavulana watatu ambao walikuwa ; Aslay, Enock Bella na Beka Flavour baadaye wakaunda kundi la Yamoto Band. Miezi michache baada ya kuanzishwa, bendi ya Yamoto ikawa jina mashuhuri Afrika Mashariki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Rayvanny Waachia Ngoma Mbili Mpya Kwa Jina ‘Kazi Iendelee’

Walishinda tuzo kadhaa pamoja na hata kuzunguka ulimwengu kwa kazi zao. Kwa pamoja walifanya nyimbo kadhaa zikiwemo; Ntakupwelepweta, Basi Ninajuta, Nisambazie raha, Cheza kwa madoido, Mkubwa na wanawe na zingine nyingi.

Walakini, mnamo 2017, timu hiyo ilivunjika baada ya tofauti zisizojulikana. Mbosso alijaribu kuwasihi wenzake wakae pamoja lakini alishindwa. Akiwa hana chochote cha kufanya katika Jiji, Marombosso alirudi kwa asili yake kijiji cha Kibiti.

Maisha ya Mbosso yalikuwaje baada ya kutoka Yamoto Band?

Baada ya Yamoto Kusambaratika , Mbosso alijaribu kurudi kwenye kilimo  ila hakufanikiwa kwa sababau umaskini ulimzidi sana. Wakati huo, hakufanya mziki tena jambo lililofanya marafiki zake kumpigia simu sana wakijaribu kumsahuri arudi mjini wengi wakiamini kuwa talanta yake ya sanaa haikufaa kuozea kijijini lakini hawakufaulu. Ila mambo yalibadilika ambapo mwendani wake Rayvanny alipochukua jukumu na kwenda kwa kina Mbosso na  kumshawishi arudi  Dar Es Salaam na ahadi ya kusainiwa chini ya lebo ya Wasafi.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Mnamo Februari 2018, Mbosso aliachia wimbo wake wa kwanza 'Nimekuzoea' kama msanii chini ya rekodi za Wasafi. Hii ilikuwa baada ya kupewa jukumu la kuandika nyimbo zote za albamu yake ya kwanza. Kwa sasa amefanya nyimbo kadhaa zikiwamo kolabo ambazo zimemrudisha kwenye hadhii ya sanaa.

Hivi karibuni alichia albamu yake rasmi kwa jina “Definition Of Love....” na imetamba kwa ukubwa sana.

Nyimbo Bora za Mbosso ni kama zipi? 

  • Nimekuzoea                     
  • Tamba
  • Haijakaa Sawa                  
  • Maajab
  • Ate                                        
  • Watakubali
  • Alele                                     
  • Picha yake
  • Shilingi ft Reekado Banks             
  • Tamu
  •  Hodari                                  
  • Nadekezwa
  • Sina Nyota

Mbosso ana uhusiano na nani?Je ana  Watoto?

Wakati alikua akifanya mziki wake wa kwanza, alikutana na mwanamke mzuri anayeitwa Rukia na akampenda. Kwa wakati huu, bado Mbosso hakuwa maarufu lakini  Rukia alikuwa tayari kuwa na Mbosso.

Mbosso hakuamini kwamba mwanamke kutoka jiji anaweza kumkubali kijana ambaye alikuwa mwizi mdogo hapo awali.

Kwa hilo, aliandika wimbo wa 'Watakubali'  ambao uliangazia maisha yake ya zamani jijini ambapo karibu apoteze maisha. Mbosso na Rukia walibarikiwa kupata mtoto na wakamwita Iqram Khan.

Miaka miwili iliyopita Mbosso alimpoteza Martha, ambaye alikua mama wa mtoto wake mwingine, na kifo chake kiligubikwa na utata si haba.

Kulingana na Mbosso ana watoto nchini Tanzania na Kenya.

Leave your comment