S2kizzy Awaalika Maproducer Wengine Kushiriki Kuitengeza Albamu ya Diamond

[Picha: S2kizzy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Producer tajika nchini Tanzania S2kizzy amewaalika maproducer wengine walio na midundo kali kuziwasilisha kwake ili wapate fursa ya kushirikishwa kwenye albamu mpya yake Diamond ilio katika harakati za kuandaliwa nchini Afrika Kusini.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, S2kizzy aliandika kuwa anaandaa albamu ambayo haitowahi kutokea kamwe kwani itakuwa ni kubwa ulimwenguni.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Producer yeyote anayejiskia kutuma beat yake atahitajika kuziwasilisha kupita barua pepe kwenye anwani ya S2kizzy.

"I’m preparing the biggest album ever in  the world @diamondplatnumz album....... as a leading producer I give chance to any producer who can send his best beats so as@diamondplatnumz can jump onto it kizzyryder95@gmail.com....” aliandika s2kizzy.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Rayvanny Waachia Ngoma Mbili Mpya Kwa Jina ‘Kazi Iendelee’

Hivi karibuni, S2kizzy alieleza kuwa yeye hufurahia kufanya kazi na Diamond Platnumz.

Akizungumza na wanahabari, S2Kizzy alisema kuwa licha ya Diamond kuwa msanii mkubwa, Simba hana tabia za kushinikiza watayarishaji wake wa muziki.

Soma Pia: Diamond Platnumz Kumshirikisha Focalistic Kwenye Albamu Yake

Kulingana na S2kizzy, anafurahiya kufanya kazi na Diamond kwa sababu anaunda mazingira bora ya kufanya kazi, akiongeza kuwa wakati wa kufanya kazi Diamond habagui yeyote.

Zaidi ya yote, S2kizzy alisema kuwa Diamond anaulewa muziki kwa kina na kila wakati huja studio akijua anachotaka, kwa hivyo kuifanya iwe rahisi kutoa nyimbo kali.

Leave your comment