Dogo Janja Kuachia Albamu Aliyowashirikisha Kina Dada Pekee

[Picha: Dogo Janja Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Dogo Ganja ametangaza ujio wa albamu yake mpya hivi karibuni.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Hii itakua ni albamu yake ya pili tangu kuanza mziki wake na itakua tayari mnamo tarehe 21, Mei, 2021.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Kupitia mtandao wa Instagram Dogo Janja ametangaza kuwa albamu yake sasa ipo tayari. Vile vile ameelezea kuwa alabamu yake itakuwa na ngoma 11 aliyo washirikisha wasanii wa kike pekee ili kuonyesha uwezo wa wanawake ulimwenguni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Rayvanny Waachia Ngoma Mbili Mpya Kwa Nina ‘Kazi Iendelee’

Haya yanajiri baada ya Dogo Janja kuwa kimya kwa muda katika mziki huku sababu yake ikiwa alichukua mwaka mmoja na siku ishirini na moja katika maandalizi ya albamu hii.

“Leo ninayo furaha kuwajulisha yakua albamu yangu ya pili tayari imekamilika na itakua sokoni kuanzia 21st May 2021..najua umenimiss hata mimi nimewamiss pia.. nimetumia mwaka na siku 21 kuandaa hii Album ambayo nimeshirikisha (WANAWAKE Tu!) ili kuionyesha Dunia kua wanawake wanaweza,Album itakua na ngoma 11,next week nitawaonyesha Track List,jina la Album na cover ya Album! Kaa karibu na mimi,” aliandika Dogo Janja.

Msani huyo ameahidi kuachia jina na orodha ya nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo wiki ijayo.

Dogo Janja ni miongoni mwa wasanii tajika nchini kwenye fani ya mziki wa rap na anashabikiwa sana.

 

Leave your comment