Diamond Aelimisha Wasanii Jinsi ya Kutengeza Pesa Mtaondoni

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kwa muda mrefu Diamond Platnumz ametumika kama kigezo katika kuelimisha wasanii namna ya kupata mauzo ya mziki. Hii leo Diamond alijitolea kutoa somo kuhusu uzaaji wa mziki kwa mfumo wa kidijitali.

Kupitia mtandao wa instagram, ameandika haya: “SOMO: Streams- Mauzo kwa njia ya Kusikilizwa, Views- Mauzo kwa njia ya Kutazamwa, Downloads -Mauzo kwa njia ya mtu kupakua….” Akiendendelea anaelezea kuwa nchini Tanzania njia ya kusambaza mziki inayotumika sana ni YouTube na mauzo yao yakiwa ni Views au usikilizaji ambayo tafsiri yake ni mauzo.

Soma Pia: Diamond Asherekea Baada ya Wimbo Wake ‘Waah’ Kupata Watazamaji Milioni 60

“Tanzania Platform inayopendwa kutumiwa na wanunuzi wetu wa Muziki ni YOUTUBE na Mauzo yao yanaitwa Views... Hivyo Mkisikia views tafsiri yake ni Mauzo Jifunzeni!” aliandika Diamond

Vile Vile Diamond alitumia fursa hiyo kuelezea moja kwa moja alivotengeza Millioni themanini na tisa kupitia wimbo wake maarufu #Waah.

“Wimbo wa #WAAH Ulipofikisha viewes Milion 39,358,770 ulitengeneza Euros 32,266.53 sawa na Shilingi Milioni 89,869,867.07 Hivyo Unaposikia Neno Views, si ujivuni tu wa watu kutazama wimbo au content...Ni Distribution sales, Mauzo kwa njia ya watu kutazama Jifunzeni !”aliandika Diamond.

Soma Pia: Wasifu wa Diamond Platnumz, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Thamani na Mahusiano Yake

Ila alionya kuwa sio kila wimbo ukifikisha views hizo unaweza ingiza kiasi hicho cha pesa.

Alisisitiza kuwa pia inategemea wimbo wako umetazamwa sana kwenye nchi ipi na ipi kwa sababu kuna baadhi ya nchi views au utazamaji wake hauiingizi kipato kikubwa.

“…Nchi zilizoendelea views zake zina kipato kikubwa kwa sababu waweka matangazo wanaweka bajeti kubwa...”aliandika.

Simba aliwasahi wasanii wenzake kujitahidi na kuhakikisha kuwa kazi zao zinafwatiliwa na nchi za nje pia.

 

Leave your comment