Afueni kwa Wasanii wa Bongo Baada ya Serikali Kukubali Warushe Kazi zao YouTube Bila Malipo

[Picha: Abbasi Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano na Teknolojia Tanzania (TCRA), wamekubaliana kubadilisha Kanuni ili wasanii na wenye maudhui ambayo sio Habari waweze kurusha kazi bila kufanya usajili na malipo kwa TCRA.

Akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) na vyama vinavyounda shirikisho hilo Jijini Dar es Salaam, katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa kufuatia kuona umuhimu wa kuwanufaisha Wasanii na kukuza Sanaa nchini.

SOMA PIA: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Wizara hizo mbili zimeafikia kubadilisha kanuni ili wasanii na wadau wengine wa maudhui yasiyohusisha usambazaji wa habari waweze kuweka kazi zao kwenye akaunti zao binafsi za YouTube bila kufanya usajili na malipo kwa TCRA.

“Tumefanya mazungumzo na wenzetu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na TCRA kuhusu maudhui ya Tv za mtandaoni, tumeona kuna tofauti kubwa sana kati ya Habari na Sanaa, hivyo tutaboresha kanuni, tumeona eneo hili la Wasanii linapaswa kufanya kazi zao bure, sasa nafurahi kuwaambia kuwa kuanzia sasa wasanii wawe wa muziki au filamu changamoto hii imefika mwisho,” amesema Dk. Abbasi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Vilie vile Abbasi amewataka Wasanii kuwa makini katika kazi zao na kutumia talanta na taaluma zao katika kutangaza kazi zao. Anaamini kuchafuliana jina katika sanaa ni kuondoa uaminifu haswa kwa mashabiki na jamii kwa ujumla ambao wameijenga kwa miaka mingi sana.

“Wote mmeona yaliyokuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni, sasa ile inaua sanaa, leo hata makampuni yaliyoanza kuwa na imani kibiashara na wasanii wameanza kusita tena, heshimuni sanaa ni maisha ya wengi na hii itawajengea heshima badala ya kutumia kiki za kuchafuana” ameongeza Dk. Abbasi.

Leave your comment