Diamond Asherekea Baada ya Wimbo Wake ‘Waah’ Kupata Watazamaji Milioni 60

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz ni mwenye furaha baada ya wimbo wake “Waah” kufikisha watazamaji millioni sitini ndani ya miezi mine.

Katika wimbo wa “Waah” Diamond alimshirikisha nguli wa mziki kutoka Congo Koffi Olomide.

Kufikia sasa, huu ndio wimbo wake mkubwa mwaka 2020 baada ya kuachiwa na kupokelewa kwa ukubwa sana.

Soma Pia: Wasifu wa Diamond Platnumz, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Thamani na Mahusiano Yake

Tangu kuachiwa, wimbo huu umevunja rekodi mbali mbali kama vile kupata watazamaji milioni moja kwenye YouTube ndani ya masaa nane.

Hii ilikuwa dhihirisho ya ubabe wa Diamond Platnumz katika fani ya mziki wa Afrika mashariki.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond Platnumz ameshukuru mashabiki kwa kumkubali huku akidokeza ujio wa kazi mpya. “#Waah 60 Million Views within 4 Months....New Song?? New Album????” Aliandika Diamond.

Huku mashabiki wakitarajia ujio wa nyimbo zingine mpya huu, haijulikani ni lini kazi hizi mpya zitakuja ila ni kusubiria tu.

Soma Pia: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Mwaka huu Diamond Platnumz hajaachia kazi yake binafsi lakini amejihusisha kwa kushirikiana na wasanii wengine.

Kwa sasa Diamond anang’ara katika ushirikiano wake kwenye wimbo wa Mbosso “Baikoko” kutoka albamu ya “Definition of Love”.

Vile vile, alihusika katika nyimbo ya kuwasifia akina mama siku ya akina mama duniani na wimbo wa kumuaga hayati rais wa Tanzania John Pombe Magufuli iliyowajumuisha wasanii tajika Tanzania.

Leave your comment