Nyimbo Tano za Rayvanny Zilizompa Umaarufu Bongo

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Msanii kutoka lebo ya Wasafi Rayvanny ni mojawapo ya wasanii wakubwa nchini Tanzania.

Licha ya kujiunga na rasmi na sekta ya muziki miaka mitani iliyopita, Rayvanny ametia bidii na sasa ni miongoni mwa wasanii tajika Afrika.

Read Also: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Kiuno’

Kufanya kazi na Diamond imemsaidia kuboresha hadhii yake barani Afrika. Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano zilizompa Rayvanny umaarufu Bongo.

Kwetu

Huu ulikua wimbo wake wa kwanza katika lebo ya wasafi. “Kwetu” ni wimbo uliongazia maisha ya kijana anayejaribu kujitafutia kipato mjini, huku mpenzi wake akitaka kujua kwao nyumbani. Kufikia sasa ni wimbo una watazamaji zaidi ya milioni 25.

https://www.youtube.com/watch?v=2uiFXUMVq5w

Natafuta Kiki

‘Natafuta Kiki’ ni wimbo wenye kuangazia namna vijana wengi haswa wasanii chipukizi hufanya ili kupata umaarufu. Wimbo huu uliachiwa miaka minne iliyopita na kwa sasa una watazamaji zaidi ya milioni 11.

https://www.youtube.com/watch?v=mOC3n5TlQH4

Mbeleko

‘Mbeleko’ ni wimbo wa mapenzi unaohusisha mapenzi kati ya watu wawili wanaopendana sana. Kuthamini upendo, Rayvanny yuko radhi kumbembeleza mpenzi wake aliyeathirika katika ajali. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamji zaidi ya millioni kumi na tano.

https://www.youtube.com/watch?v=PPT1MgfwArE

Read Also: Nyimbo Mpya: Diamond Atamba Kwenye Orodha ya Nyimbo Kumi Bora Mdundo Tanzania

Zezeta

Huu ni wimbo unaashiria uzuri wa upendo ulio na thamani, kuaminiana na kujali maslahi ya uliye naye. Ni wimbo uliotengezwa miaka mitatu iliyopita na unawatazamaji zaidi ya millioni tisa.

https://www.youtube.com/watch?v=C_cp5lJ6VY4

Unaibiwa

Huu ni wimbo unaongazia wazee walio na michepuko. Rayvanny anawaonya watu wa umri mkubwa kutochepuka na akina dada wadogo. Ni wimbo ulio na watazamaji milioni kumi na moja kufikia sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=Pb3adebbryg

Leave your comment