Nyimbo Tano za Mapenzi Kwa Ajili ya Siku ya Wapendanao [Video]

[Picha: Standard]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Mwezi Februari unajulikana kuwa mwezi wa mapenzi. Hivo siku ya wapendanao almaarufu -Valentine's Day –inapokaribia, tumekuandalia orodha ya nyimbo za mapenzi kutoka Bongo unazofaa kuskiza na mpenzi wako:

Soma Pia: Jux Arejea na Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘Sio Mbaya’

Sawa - Juma Jux

Jux aliachia wimbo wa ‘Sawa’ hivi karibuni. ‘Sawa’ ni wimbo wake wa kwanza mwaka huu. Juma ameachia wimbo huu kama adhimisho ya mwezi wa mapenzi. Wimbo huu unaingia kwenye orodha hii kwa sababu ya ujuzi wa Jux kwenye nyimbo za mapenzi na RnB.

Download Juma Jux Music For Free on Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=zs28UF30QWY

Dodo - Alikiba

Ni wimbo wake Alikiba unaoangazia maana kuu ya upendo ambayo ni vitendo na si maneno tu. Wimbo huu ni mzuri kwa wapenzi wachanga kwa utawaisidia kustawisha mapenzi yao.

Soma Pia: Jux Biography, Music Career, Awards, Net worth and Break Up with Vanessa Mdee

https://www.youtube.com/watch?v=1h3VzH-I7b8

Waaah - Diamond Platnumz na Koffi Olomide

‘Waah’ Ni mojawapo wa nyimbo maarufu barani Africa. Diamond alimshirikisha Koffi Olomide katika wimbo huu ambapo wanamsifia mpenzi wake. Katika maisha ni wengi wanatamani kuwa na mtu atakaefurahia uhusiano wao. "Waah" basi ndio wimbo wa kutumia katika kumteka unayempenda.

https://www.youtube.com/watch?v=HCuTwNgY3_M

Wivu - Mausama na Aslay

Huu Ni wimbo unaoangazia changamoto ya wapenzi wanaoshirikiana kufanya mapenzi yao kunawiri. Mausama anamshirikisha Aslay ambapo anamsifia mpenzi wake kwa ujuzi wake kwenye jikoni. Hii ikiwa namna ya kuwahimiza watu kutofanya wivu iwe kigezo cha kuvunja mapenzi yao.

Number One - Rayvanny na Zuchu

Wimbo huu unamaudhui mazito ya mapenzi ambapo Zuchu na Rayvanny wanaelezea kwa nini mpenzi wao ni nambari moja. Huku Zuchu akisema moyo wake hausukumi damu tu ila upendo wake kwake Rayvanny. Wawili hao walifanya wimbo huu mahususi kwa ajili mwezi kama huu wa mapenzi.

 https://www.youtube.com/watch?v=8bQOuK95uYQ

Leave your comment