Nyimbo Mpya: Juma Jux Aachilia Ngoma Mpya Kwa Jina ‘Sawa’

[Anwani ya Picha: Juma Jux Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Share on WhatsApp

Msanii wa mziki ya aina ya RnB Juma Jux ameachilia wimbo wake mpya kwa jina ‘Sawa’.

‘Sawa’ ni wimbo wake wa kwanza mwaka huu. Juma ameachia wimbo huu kama adhimisho ya mwezi wa mapenzi.

Soma Pia: Jux Biography, Music Career, Awards, Net worth and Break Up with Vanessa Mdee

“Huna kama acha mapinzani, Kila siku matatizo, Inanidhiri ndani wa ndani, Naikosa Chanjo Oo hoo, acha visa nazo unanikula moyo, usingizi sipati , kisa kwako sipati maamuzi…” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Jux anaendelea kuweka wazi kuwa upendo anaouhisi ni mkubwa sana ila tu hajui vile ya kufanya maamuzi yake.

Download Juma Jux Music For Free on Mdundo

‘Sawa’ ni kumbusho kwa mashabiki kuthamini mapenzi walionayo na kuwapenda wapenzi wao bila masharti yoyote.

Kufikia sasa Jux ameachia tu audio ya wimbo na imepokelewa vizuri sana. Wimbo huu umetengezwa na producer maarufu Bob Manecky.

Soma Pia: Jux Arejea na Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘Sio Mbaya’

Kanda ya wimbo huu inatarajiwa hivi karibuni. Jux ameendelea kukuza mziki wake bila kusita na hivi karibuni anatarajiwa kuwa na tamasha kubwa kwa jina ‘The Finest’ nchini Kenya mnamo tarehe 14 Februari ambapo atakua pamoja na Otile Brown, Nikita Kering na Samidoh.

https://www.youtube.com/watch?v=QrLJcXUt7YU

Leave your comment