Harmonize Kuachia Collabo na Master KG wa Afrika Kusini

[Photo Credit:Music in Africa]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mkurungenzi mkuu wa Konde Music Worlwide Harmonize hivi karibuni ataachiawimbo mpya akimshirikisha msanii kutoka Afrika kusini almaarufu Master KG.

Master KG anajulikana kwa wimbo wake maarufu “Jerusalema” aliomshirikisha Nomcebo.

Hivi maajuzi, msanii huyo amekua nchini Tanzania kwa ajili ya tamasha iliyokuwa imeandaliwa na Cloulds FM kwa jina 'Life’s a Breeze’.

Soma Pia: Harmonize Reveals How Much he Earns for Every Performance

Akizungumza wakati wa mahojiano na Clouds FM, Master KG alimsifu Harmonize akisema kuwa ndiye rafiki yake mkubwa nchini Tanzania na kwamba wawili hao wanafanya kazi pamoja.

Kupitia mtandao wa Instagram, Harmonize aliweka picha kwenye akaunti yake wakirekodi wimbo wao ambao mashahbiki sasa waingoja kwa hamu.

Harmonize kwa upande wake alikua mwenye furaha sana akisema Master KG amempea bonge la mwaka mpya.

Hivyo basi inataraijwa kuwa wimbo huu utaachiwa mwakani. Utakumbuka kuwa wasanii hawa wawili wana umahiri mkubwa barani Afrika.

Master KG atakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kusini kushirikiana na Harmonize.

Soma Pia:  Harmonize Biography, Music Career, Wasafi Exit, Starting Konde Gang, Top Songs, Relationship and Net worth

Kwingineko, kufuatia wimbo wake ‘Jerusalema’ kuwa mkubwa kote ulimwenguni, Master KG mwaka 2020 ndio msanii aliyetafutwa sana kwenye mtandao wa kutafuta mziki almaarufu Shazam.

Vile vile kwenye tamasha hilo la ‘Life’s a Breeze’, Harmonize alichukua fursa kuwaeleza mashabika hela anazopata kila akipanda jukwani kuwatumbuiza.

Kulingana na Harmonize, yeye hulipwa dola elfu 25,000 (milioni 57 hela ya Tanzania).

Leave your comment