Diamond Amshusha Harmonize Kwenye Orodha ya Nyimbo Bora Mdundo Tanzania

[Photo Credit:Diamond Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz anaendelea kupata umaarufu zaidi baada ya kuachia wimbo wake “Waah” ambao alimshirikisha msanii wa Congo Koffi Olomide.

Kufikia sasa kwenye orodha ya nyimbo kumi bora kwenye mtandao wa Mdundo Tanzania, Diamond amemshusha Harmonize kutoka nambari moja hadi ya tatu.

Diamond ameweza kuchukua nambari moja, sita, na ya kumi.

Download Diamond Music for Free on Mdundo

Nyimbo za Diamond zilizo kwenye orodha hii ni Waaaah,Jeje na Haunisumbui.

Harmonize amekua akishikilia nambari moja kwa muda mrefu na leo ana wimbo mmoja tu wa “Ushamba” kwenye orodha hii.

Kwingineko, orodha hii imetawaliwa na wasanii kutoka Nigeria ambao ni; Simi, Rema, Patoranking na Joeboy huku wimbo wa Msanii kutoka Afrika Kusiani Master KG ukiendelea kuwa kwenye orodha hii.

Soma Pia: Diamond Releases New Hit Dubbed ‘Waah’ Featuring Koffi Olomide

Orodha ya nyimbo hizi ni kama ifuatavyo:

  1. Waaah - Diamond Platnumz ft Koffi Olomide
  2. Jerusalema - Master KG ft Nocebo
  3. Ushamba - Harmonize
  4. Baby - Joeboy
  5. Duduke - Simi
  6. Jeje - Diamond Platnumz
  7. Jericho - Simi ft Patoranking
  8. Remember Me - Lucky Dube
  9. Ginger Me - Rema
  10. Haunisumbui - Diamond Platnumz

Leave your comment