Video Tano Bora Zaidi zake Lava lava

[Picha: Lava Lava Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii wa Wasafi Lavalava ni mojawapo wa wanamuziki wanaoheshimika nchini Tanzania. Kwa miaka karibu minne ndani ya lebo ya Wasafi ameweza kuachia mziki ambao wengi wameipokea vizuri sana. Hata akiendelea kujitahidi kuachia nyimbo zingine, katika nakala hii tunaangazia nyimbo tano bora amewahi kufanya Lavalava.

Tuachane

Huu ulikua wimbo wake wa kwanza kabisa alipojulishwa kwa mashabiki miaka mitatu iliyopita. ‘Tuachane’ ni wimbo ambao mwanamume amevunjwa moyo na mpenzi wake wa muda mrefu. Lavalava anaelezea namna alivyochoshwa na mwanamke anamchukulia fala katika mapenzi. Kufikia sasa wimbo hiuu bado unaenziwa na mashabiki na unawatazamaji zaidi ya milioni kumi na tatu.

https://www.youtube.com/watch?v=BJ9FLAnEUg4

Dede

‘Dede’ ni wimbo aliouachia kwa ajili ya kumsifu mpenzi wake. Lavalava anaelezea namna anavyompenda mpenzi wake ‘Dede’ na hataki mwingine kwani huyu anamkamilisha kimapenzi. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa kwa zaidi ya mara milioni nne nukta sita.

https://www.youtube.com/watch?v=FvShlGAk6vk

Niuwe

Wimbo huu nii wenye staha huku Lavalava akimsifia msichana anayempenda kuwa maumbile yake yanamridhisha yeye. Wimbo huu pia ulipokelewa vizuri na mashabiki na kufikia sasa umefikisha watazamaji zaidi ya milioni kumi na moja miaka miwili baadae.

https://www.youtube.com/watch?v=YBHbK-ZPo_c

Soma Pia: Read Also: Lava Lava Releases New Song ‘Ipekeche’

Gundu

‘Gundu’ ni wimbo wenye hisia kali za mapenzi. Huu ni wimbo ambao Lava Lava anashangaa namna mapenzi yanamtonesha kidonda kila kukicha. Gundu ni wimbo ambao mashabiki wengi walifurahia kwani mistari ya wimbo huu iliwagusia wengi waliopitia mashaka katika mapenzi. Kufikia sasa wimbo huu unawatazamaji zaidi ya milioni tisa.

https://www.youtube.com/watch?v=bmVXA2CXitI

Go Gaga

Ni wimbo aliochia miaka miwili iliyopita anapomsifu mwanamke anayempenda kwa mauno aliyonayo. Lavalava anamwambia mpenzi huyo aonyeshe uwezo wake watu waone huku yeye akimfanya apagawe. Wimbo huu unawatazaji zadi ya milioni sita.

https://www.youtube.com/watch?v=9_4RXAg4pqk

Soma Pia: Ben Pol Amsifu Barnaba, Amtaja Kuwa Chuma ya Mziki wa Tanzania

Leave your comment