Koffi Olomide Amsifu Zuchu na Kumtaja Mmoja wa Wasani Tajika Afrika

[Photo Credit: Zuchu and Kofi Olomide Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msanii kutoka lebo ya Wasafi Zuchu anaendelea kupata sifa kutoka kwa wasani tajika barani Afrika. Hivi karibuni Zuchu amepata kusifiwa na msanii gwiji kutoka Congo Koffi Olomide.

Muimbaji huyo akizungumza kwenye kipindi cha the The Switch katika kituo cha Wasafi Fm, alisema kuwa alistaajabishwa na kipawa na uwezo wake Zuchu.

Aliongezea kuwa mkurungenzi mkuu wa wa WCB Diamond Platnumz anajua kutambua talanta anapoiona.

Soma Pia:Diamond Releases New Hit Dubbed ‘Waah’ Featuring Koffi Olomide

“Today I have discovered another female singer produced by Diamond’s label she sang for me ….ahhh Zuchu…aahhh wawa wa wa!!I ma very happy for Africa. If you are listening I say Congratulations. First time I heard her sing her voice her style, she is the voice of Africa. I say she stay with Diamond to Grow…” Koffi alisema kwa kifupi.

Kwa upande wake Zuchu alitoa shukrani kwa Koffi kumpa sifa haswa kwa tajriba ya ujuzi wake kwenye fani ya mziki.

Soma Pia:Zuchu Drops New Emotional Song Dubbed ‘Hasara’

"Oh My God !!Thank you so much @koffiolomide_officiel Mopao for these comments. when I sang there didn’t even know It would turn to such beautiful comments .Merci .KING .The king of Africa complimented me today Wow .Somebody wake me up Super grateful," aliandika Zuchu.

Koffi Olimide amekuwa nchini Tanzania wiki akifanya kazi na Diamond Platnumz. Pamoja wameachia wimbo mpya almaarufu "Waaah".

Kwa upande mwingine, alikuwa nchini Tanzania kufanya video ya wimbo wake utakaoachiwa tarehe 28 Novemba 2020.

Koffi ameipongeza timu ya Wasafi kwa maadili yao ya kufanya kazi ambayo yamemvutia. Kufikia sasa, ushirikiano wake na Diamond Platnumz umekuwa na umuhimu mkubwa kwani vizazi viwili tofauti kuja pamoja kufanya mradi huo mkubwa sio kitu rahisi.

Leave your comment