Diamond Kuachia Ngoma Mpya na Koffi Olomide

[Anwani ya picha:Diamond Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mkurugenzi mkuu wa lebo ya Wasafi Diamond Platnumz amemkaribisha msanii mkubwa kutoka Congo Koffi Olomide nchini Tanzania kwa minajili ya kufanya kazi pamoja.

 Akipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, mwimbaji Koffi Olomide alikaribishwa kwa heshima kubwa na alipata fursa ya kuzunguza na wanahabari kuhusu safari yake nchini Tanzania.

“I’m here to work with Diamond …uuuh to do something to amaze Africa and the world and am sure it will be a very big success. My matter is music his matter is music so we are doing music together…” alisema kwa kifupi.

Soma Pia: Zuchu Ateuliwa Balozi wa Kampuni Kubwa Tanzania

Koffi alielezea kuwa yuko Tanzania kwa heshima ya Diamond Platnumz ambaye amefanya vizuri sana kuupa mziki wa Afrika hadhi kote ulimwenguni.

Download Diamond Music for Free on Mdundo

Msanii Olomide alimtaja Diamond Platnumz kama mfalme wa mziki nchini Tanzania huku mwimbaji huyo wa “Haunisumbui” akijishusha na kujiita “Prince” (mtoto wa mfalme).

Kufikia sasa, wawili hao wamekwisha ingia kwenye studio kurekodi wimbo wao ambao  unatarajiwa kwa hamu na mashabiki.

Soma Pia: Rayvanny Asherekea Wimbo wake ‘Tetema’ Kufikisha Watazamaji Milioni Tisini

Mwanmziki Koffi anatarajiwa kusherekea miaka 30 katika fani ya mziki mnamo mwezi wa Februari mwaka 2021.

Koffi ni msanii anayeendelea kuachia mziki kila kukicha na wengi wetu tumekua tunafurahia mziki wake kupitia kwa wazazi wetu waliomuenzi mwanziki huyu kutoka Congo.

 

Leave your comment