Harmonize Azua Tetesi Mtandaoni Baada ya Kuposti ‘Malegend wanahofia Jeshi’

[Photo Credit:Harmonize Instagram]

By Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mwanzilishi wa lebo ya Konde gang worldwide Harmonize amezua gumzo mtandaoni hivi maajuzi baada ya kuandika ujumbe tatanishi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ujumbe huu umepata tafsiri tofauti miongoni mwa mashabiki wake Harmonize, wengi wakisema kua ni wimbo mpya unaotarajiwa kutoka kwa mwimbaji huyo wa Konde Gang.

“Malegend wamerudisha viti eti wanahofia jeshi anawapita bila sababu wananikunjia ndita eeh huo ni Ushamba,” aliandika Harmonize.

Chini ya ujumbe huo , neno “Ushamba” limeandikwa tena kivyake hivyo mashabiki wanaamini kuwa Harmonize atakua anaachia ngoma yake mpya.

Hii ni licha ya kutotoa ujumbe rasmi kuhusu aliyo andika. Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Harmonize alitikisa mtandao wa Instagram aliposema wimbo wake mpya utawatishia wengi.

Download Harmonize Music for Free on Mdundo

Haijulikani ni lini haswa kitafanyika lakini Harmonize alianza kwa kuandika kuwa; "Tarehe 1-11-2020 Siku ya Washamba Duniani”.

Kupitia maneno haya Harmonize ameacha pengo kwa mashabiki huku kila mmoja akijaribu kutupa tafsiri yake namna alivyoeleewa ujumbe huo.

Kwa sasa Harmonize anatamba katika wimbo aliyoshirikiana na msanii wa lebo yake Country wizzy “Far away” ambao unaendelea kupata umaarufu kwenye mitandao ya mziki.

Wiki chache zilizopita, mkuu wa lebo ya Kings Records Alikiba alitumia namna hii ya kuandika mtandaono vipengee vidogo vidogo vya kustukiza kabla ya kuachia ngoma yake ya “Mediocre”.

Leave your comment