Mbosso Aomboleza Kifo cha Shabiki Wake Mkongwe Kutoka Kenya

[Anwani ya Picha: Instagram Lamu Confuse]

Mwandishi: Branice Nafula

Follow Us on Google News

Mwanamziki kutoka Wasafi Mbosso ni mwenye huzuni baada ya kupata habari ya kuhuzunisha kuwa shabiki wake mkongwe kutoka Kenya ameaga dunia.

Mboso alibahatika kuwa na uhusiano wa karibu na shabiki huyu mkongwe kutoka Lamu ambapo aliweza kuupa wimbo wake Mbosso “Shillingi” umaaraufu zaidi kisiwani Lamu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbosso amemuomboleza Mzee Janizo almaarufu Lamu Confuse.

Mbosso amemtaja Janizo kama shabiki aliyempa yeye nguvu ya kufanya kazi nzuri zaidi.

“Mwenyezi Mungu amenipa bahati ya kuwa na Mashabiki wengi sana wa rika tofauti tofauti , ila kupata Mashabiki wenye Umri zaidi Ya Baba Yangu au Babu yangu ni bahati kubwa na ya Kipekee Sana Kwangu Kupitia Wewe Ulifanya Wimbo wangu wa Shilingi Kuwa wimbo namba Moja Kisiwani Lamu Kenya na Ukawafanya Viongozi na Wananchi Wa Kisiwa Cha Lamu Kenya wakawa Mashabiki Wangu Wakubwa sana .. Ulikuwa zaidi Ya Shabiki Kwangu .. ulikuwa Kama Mzazi wangu ..Nimeumia sana Leo Mzee Wangu @lamu_confuse umeniacha ..Mwenyezi Mungu akupe Kauli thabiti , Akuweke Kwenye Pepo Yake ya Firdausi kwa baraka zake na huruma yake Inshaallah na akusamehe makosa yote Inshaallah Maana Yeye ni Mwingi wa huruma na mwenye kusamehe,Pumzika kwa Amani Mzee Wangu wa Shilingi Ya ng'ara ng'ara Lamu Confuse @lamu_confuse Mzee wa Nipepee alitangulia .. na Wewe Umemfatia "Innalillah Wainnailah Raajuun,” he posted.

Leave your comment