Zuchu Atajwa Mwanamuziki wa Kike Aliyesikilizwa Zaidi Afrika Mashariki

[Anwani ya Picha: Afroway]

Mwandishi: Branice Nafula

Follow Us on Google News

Msaani kutoka lebo ya wasafi Zuchu anaendelea kupata umaarufu zaidi ulimwenguni kupitia kazi yake bora.

Baada ya kuwa na kazi nzuri za mziki Zuchu sasa ni msanii wa kwanza wa kike kupata wasikilizaji milioni saba kwenye mtandao wa boomplay.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zuchu aliwashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kuskiza mziki wake.

Vile vile aliahidi kuendelea kuachia mziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wake.

“Msanii wa Kwanza wa kike East Africa kufikisha wasikilizaji 7,000,000 million on @boomplaymusic_tz Asanteni sana kwa upendo huu usio elezeka Nawapenda sana I’ll keep working hard for you my supporters .Ndo kwanza Nimeanza we have a list to accomplish.I LOVE YOU,” Zuchu aliandika.

Zuchu anaendelea kudhihirisha umahiri wake kweneye fani ya Bongo flava miezi saba baada ya kutambulishwa kwenye lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Hatua hii mpya ya Zuchu inampa changamoto ya kuwa na bidii zaidi ya kuendelea kufanya kazi nzuri.

Lebo ya Wasafi kupitia viongozi wake hawana shauku na uwezo wa Zuchu hivyo ushirikiano wao katika kazi mbali mbali umempa Zuchu motisha ya kufanya vizuri.

Sasa hivi, Zuchu ni mojawapo wa wasani tajika Afrika nzima na amepata kushirikiana na wasanai wakubwa kama vile Joeboy wa Nigeria na wengineo.

 

Leave your comment