TANZANIA: Kubaki Local au Kwenda International ni Uamuzi wa Msanii Mwenyewe - AY

AY ni msanii wa kwanza kutoka Bongo kuwekeza muziki wao nje ya nchi kwa kufanya kazi na wasanii wakubwa kwa wakati huo akiwemo Ms Triniti, Sean King Stone na P Square. Rapper huyo amefunguka kuwa kufanya hivyo inategemea na malengo ya msanii mwenyewe.

AY amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, kuna baadhi ya wasanii wana malengo ya muziki wao kufika nje lakini wengine malengo yao ni kufanya vizuri ndani ya nchi pekee.

“Msanii kuwekeza muziki wake nje au ndani ya nchi yake ni kutegemea na yeye mwenyewe anachokitaka. Kwa sababu kuna wasanii ambao wanataka kuhit humu humu ndani ya nchi na kuna mtu anataka kujiongeza labda anataka kuhit ndani na anataka kukutana na challenges na kushindana na miziki mingine ya nje,” amesema AY.

“Inategemea na mtu plan zake anatakaje. Ni kama unavyosema watu wa football kuna mtu anataka kucheza ligi za ndani tu na kuna mtu mwingine anasema mimi nataka kucheza mpaka kufika Barcelona,” ameongeza.

Source: bongo5.com

Leave your comment