TANZANIA: Ndoto yetu mwaka huu ni kwenda Billboard na Grammy – Navy Kenzo

 

 

 

Wanamuziki wanaounda kundi la Navy Kenzo ‘Aika na Nahreel’ wamesema kuwa mipango yao ya sasa ni kwenda kwwenye chart za juu za muziki duniani kama Billboard pamoja na tuz za Grammy.

Navy Kenzo ni moja kati ya makundi yanayoshindania tuzo za MTV  Africa Music Award ‘MAMA’, zinazotarajia kufanyika tarehe 22 Octoba mwaka huu nchini  Afrika Kusini.

Katika mahojiano yao na kipindi cha The Playlist cha Times Fm Jumamosi hii, wasanii hao walisema kuwa kwa sasa wameshafanya kolabo na wasanii wa Afrika ambapo nyimbo hizo zitaweza kuwatangaza vizuri Afrika.

“Tutegemee kolabo zaidi na wasanii wakubwa duniani, ndoto yetu mwaka huu ni kwenda Billboard, kwenda Grammy na kufanya vitu vikubwa zaidi, kwa hiyo tunashukuru Mungu connetion zinazidi kuwa kubwa,” alisema Aika.

Kundi hilo mpaka sasa lina kolabo na Patoranking pamoja na Bana Boy wa Nigeria ambazo hazijatoka mpaka sasa.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news