TANZANIA: Trey Songz atua Nairobi kushiriki Coke Studio msimu wa nne

 

 

Muimbaji wa RnB kutoka Marekani, Trey Songz ametua mjini Nairobi, Kenya kushiriki kwenye msimu wan nne wa kipindi cha Coke Studio Africa.

Muimbaji huyo anatarajiwa kurekodi nyimbo na baadhi ya wasanii wengine wa Afrika ambao watashiriki kwenye kipindi hicho akiwemo Vanessa Mdee (Tanzania), Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashinski (Kenya) na Emtee (South Africa).

 

Trey Songz akila chakula cha mchana na washiriki wengine wa kipindi cha Coke Studio

 

 

 

Uongozi wa kipindi hicho umeandika ujumbe kwenye mtandao wao wa Instagram unaosomeka, “Welcome to Nairobi Kenya Trey Songz, it is a great honour to host you for #cokestudioafrica.”

Hii ni mara ya tatu kwa msanii kutoka Marekani kushiriki kwenye kipindi hicho, wengine waliowahi kushiriki ni pamoja na Wyclef Jean na Ne-Yo. Kupitia App yako ya mdundo.com unaweza kujipatia nyimbo za msimu wa 3.. Pakua sasa uweze kuburudika.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news