TANZANIA: Harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy, zinanipa nguvu kufanya kazi na Trey Songz – Vanessa Mdee

 

 

Vanessa Mdee ana ndoto kubwa. Ndoto yake siku moja, kuwa msanii kutoka Tanzania atakayeshinda tuzo za heshima, Grammy.

Na sasa anaamini kuwa, mwanzo wa kukaribia kuiishi ndoto hiyo umewadia. Vee Money, ni mmoja wa wasanii wa Afrika, waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na nyota wa RnB nchini Marekani, Trey Songz. Shukrani kwa kipindi cha Coke Studio Africa (International Week) msimu wa 4, kinachomdondosha staa huyo.

Akiwa pia anawania tuzo ya Loeries za Afrika Kusini kwa kazi yake ya video bora, Niroge, Vanessa anaungana na Rema Namakula (Uganda), Yemi Alade (Nigeria), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), Nyashinski (Kenya) na Emtee (South Africa) kurekodi wimbo na Trey Songz.

“Katika harakati zangu za kutafuta ushindi wa Grammy katika career yangu ya muziki, inanipa nguvu kufanya kazi kwa ukaribu na Trey Songz, ambaye alishawahi kushinda tuzo hiyo,” amesema Vanessa. Msimu mpya wa Coke Studio utaanza mwezi ujao na kupitia app yako ya Mdundo unaweza kusikiliza msimu wa 3, top 10 za coke studio za Tanzania na Ugandapamoja na Coke Studio Radio Hour…

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment