TANZANIA: Barakah Da Prince amekiri kuwa lugha ya Kiingereza kwake ni tatizo

 

 

 

Msanii wa muziki Barakah Da Prince amekiri kuwa lugha ya Kiingereza kwake ni tatizo huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu wa kumfundisha.

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Nisamehe’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha AliKiba, amesema katika interview yake kubwa iliyopita na MTV aliomba kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha ambayo anaweza kuizungumza.

“Niliulizwa kwenye interview ya MTV kama naweza kuongea Kiingereza, nilichowajibu naweza ila sio Kiingereza kilichonyooka ndio maana nikatumia Kiswahili. Nafurahi kwa kuwa walivutiwa na Kiswahili,” Barakah alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM Jumanne hii.

Pia muimbaji huyo amesema mpenzi wake wa sasa Naj ameshindwa kumfundisha huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu.“Hanifundishi lugha kwa sababu tuna masihala mengi hivyo nahitaji mtu ambaye atakuwa serious,” alisema Barakah.

Diamond ni miongoni kati ya wasanii ambao walikuwa hawajui kuongea lugha ya Kiingereza lakini alijifunza na sasa anakichapa kama kawaida.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment