TANZANIA: Nachelewa kutoa ngoma sababu nataka ngoma iwe nzuri na bora- Baraka Da Prince

 

 

Msanii wa Bongo fleva kutoka kwenye lebo ya Rockstar 4000, Baraka The Prince baada ya kimya cha muda mrefu, leo ametoa wimbo wake ambao amemshirikisha Ally Kiba

Enewz imepata nafasi ya kuzungumza nae juu ya kuchelewa kutoa kazi zake na je hiyo inauathiri kiasi gani!

Baraka The Prince alisema uongozi wake haupo hapa Tanzania, bali uko Afrika Kusini na wako makini hawakurupuki kuachia ngoma lazima kuwe na mikakati iliyo bora ili waweze kutoa kitu ambacho kitakuwa bora kwa sababu yeye ni msanii wa kimataifa ili afanye vizuri ni lazima atengeneze kitu kizuri.

“Management yangu haiko hapa iko South Africa na wako makini sana katika kutoa ngoma kwa sababu mimi ni msanii wa kimataifa na nataka nikitoa ngoma iwe nzuri na bora ndio maana mimi kidogo nachelewa kutoa ngoma zangu” alisema Baraka.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news