TANZANIA: Ben Pol kuja na remix ya “Moyo Mashine” akishirikiana na Chidinma

 

 

 

Msanii Ben Bol ameendelea kuupa hadhi wimbo wake wa moyo mashine, ambao ametangaza kuja na remix yake hivi karibuni, aliyomshirikisha msanii wa Nigeria Chidinma.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ben Paul amesema wimbo huo ulichaguliwa na wasanii wawili wakubwa wa NIgeria ili kuufanyia collabo, lakini kwa vile alishaufanyia mpaka video, ikashindikana kuwaweka na hatimaye kumuweka Chidinma kwenye remix yake.

"Chidinma yeye nilimpa nyimbo kama nne, kabla ya moyo mashine haijatoka, nilimsikilizisha kama nyimbo nne hivi, akachagua moyo mashine, nikamwambia moyo mashine nimeshaishoot na video na nakaribia kutoa akasema tunaweza tukafanyia remix, kwa hiyo usi-understimate mtu akichagua kitu msanii mkubwa kama yule, alafu 'same thing' kilitokea kwa Banky W na yeye nilimsikilizisha kama nyimbo nne hivi, naye akasema nataka moyo mashine, nikamwambia moyo mashine Chidinma ameitaka, kwa hiyo yeye ndo naweza nikafanya naye kitu kingine", alisema Ben Paul.

 

Chidnma

 

Ben Paul aliendelea kusema kuwa kinachochelewesha kuachiwa kwa collabo hiyo ni ratiba zilizowabana kati ya wasanii hao wawili, ambapo kila mmoja yuko busy na kufanya shows na tour.

"Sasa hivi tunajaribu ku'finalize' schedule za kufanya video, kwa sababu mi mwenyewe nafanya shows nafanya moyo mashine tours, na bi dada naye ana tour yake yuko Paris hivi karibuni, kwa hiyo tunajaribu kuangalia tupate timing nzuri kufanya video wimbo utoke kwa sababu wimbo umeshaisha", alisema Ben Paul.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news