TANZANIA: Billnas asitisha muziki kwa muda mfupi ili kuweka mambo sawa ya masomo

 

 

 

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Billnas amelazimika kusitisha kwa muda shughuli za muziki wake ili kuweka mambo sawa katika chuo anachosoma.

Rapper huyo ambaye anabukua katika chuo cha College of Business Education (CBE) jijini Dar es salaam amepata supp tatu katika baadhi ya masomo yake.

Akiongea na Bongo5 meneja wa rapper huyo, Mchafu Chakoma amesema Billnass wiki hii atakuwa busy kwa ajili ya maandalizi ya kufanya supplementary zake.

“Billnass wiki anahitaji muda mwingi wa discussion kwa ajili ya supp zake, amepata supp tatu na baada ya wiki moja atarudi kwenye mishe za muziki,” alisema Mchafu. “Yaani hajapata maksi ambazo zilikuwa zinahitajika katika hayo masomo yake, anatakiwa kupata maksi zaidi ya 40, sasa amepata chini ya hapo kwa hiyo amelazimika kurudia mitihani,”

Chakoma amesema yeye kama meneja wa LFLG, atahakikisha Billnas anaendelea kufanya vizuri katika masomo na muziki.

“Mimi nimeanza kumsaidia Billnas hata kabla hajaanza muziki, kwa hiyo wakati anasoma ndo akaniambia broo nataka kufanya muziki, mimi nikamwambia kama unaweza poa, na wakati anaanza hatukuwa tunafanya muziki kama biashara kwa sababu tunajua kijana bado anasoma,” alisema Chakoma.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment