TANZANIA: Wimbo wa Babu Talent ni Jipu - Nikki Mbishi

 

Rapa Nikki Mbishi maarufu kama 'Unju' amefunguka na kusema kuwa meneja wa wasanii Babu Tale ni jipu ambalo Rais Magufuli pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye hawawezi kuliona serikali ya awamu ya tano itakapomalizika

Rapa Nikki Mbishi maarufu kama Unju amefunguka na kusema kuwa meneja wa wasanii Babu Tale ni jipu ambalo Rais Magufuli pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye hawawezi kuliona hadi wanamaliza msimu wao wa serikali ya awamu ya tano.

Nikki Mbishi amesema anatarajia kuachia wimbo wake mpya alioupa jina la 'Babu Talent' ambao mashairi yake yanaonekana kumchana meneja wa kundi la Tip Top Connection na kudai kuwa meneja huyo ni jipu, na halitaweza kutumbuliwa katika awamu ya tano ya Rais Magufuli.

"Naitwa Babu talent a.k.a jipu ambalo Magufuli na Nape Nnauye hawataliona mpaka wanamaliza uongozi wao" alindika Nikki Mbishi

Katika baadhi ya mistari ya Nikki Mbishi inaonesha kuwa Babu Talent ndiyo chanzo cha baadhi ya wasanii kupotea kimuziki licha ya wasanii hao kuwa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye muziki.

"Ningekuwa na roho nyepesi ningeshavuta unga, Babu Talent nishampoteza hadi Daz Baba siyo kama siyo mkali ila nimeamua tu" aliandika Niki Mbishi

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news