TANZANIA: Aika Wa Navy Kenzo yuko mbioni kurudi shuleni kuongeza elimu zaidi

 

 

 

Msanii anayeunda kundi la Navy kenzo Aika Marealle maarufu kama AIKA anafikiria kurudi tena shule ili kuongeza elimu zaidi,Msanii huyo ambaye kwa sasa ana degree ya biashara ambayo alisomea India amesema hayo mara baada ya kupewa nafasi ya kutoa speech fupi kwa wanafunzi wa sekondari ya mwendakulima iliopo kahama walipofanya ziara na wasanii wengine ilikuweka msisitizo kwenye elimu kabla ya show ya fiesta iliyofanyika usiku katika viwanja vya kahama.

 

 

 

 

“Mimi ni msanii na nimesoma masomo ya biashara, nina degree lakini pia nitasoma zaidi kupata Masters hadi PhD. Sanaa ni biashara na kusoma kunakuongezea maarifa, naomba muwaheshimu walimu wenu na wazazi wenu” alisema AIKA. Aidha msanii huyo amewashukuru mashabiki pamoja na wakazi wa Kahama kwa mapokezi yao pamoja na ushirikiano waliouonyesha.

Pia Unaweza kuwapigia kura Navy kenzo katika tuzo za African Youth Choice Award kwa kupitia link hii hapa chini

http://www.africayouthchoiceawards.org/vote/best-song-http://www.africayouthchoiceawards.org/vote/best-song-by-a-duo-group-or-featu

Chanzo:Dj Choka

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news