TANZANIA: Mimi sipo 'comfortable' kuzungumza mambo yangu binafsi kwenye mitandao – Ben Pol

 

 

 

 

Msanii wa Bongo Fleva nchini Ben Pol amesema hayupo tayari kuweka bayana mambo ya kifamilia katika mitandao ya kijamii au kwenye chombo cha habari kwa kuwa haamini kama kufanya hivyo kutamsaidia.

Ben Paul ameyasema hayo katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa ambapo msanii huyo alifika kutambulisha ngoma yake mpya aliyofanya na Stereo inayokwenda kwa jina la 'Shilingi'

Baada ya kutambulisha ngoma hiyo alitakiwa kufafanua tetesi kwamba ana mgogoro wa kifamilia na mama wa mtoto wake jambo ambalo Ben Pol amegoma katu katu kuzungumzia jambo hilo kwenye media.

''Mimi sipo 'comfortable' kuzungumza mambo yangu binafsi kwenye mitandao hivyo kuhusu hizo habari sisemi chochote'' Amesema Ben Pol.

Aidha msanii Stereo amewataka mashabiki wa muziki kuisapoti ngoma hiyo ya 'Shilingi' kwa kuwa ina ujumbe maalum kwa jamii.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment

Other news