TANZANIA: Nahreel na Aika kuanza ujenzi wa nyumba yao itakayogharimu shilingi milioni 700.

 

Msanii wa Bongo Flava anayeunda kundi la 'Navy Kenzo' Nahreel amewataka wasanii kufanya mambo ya maana wanapofanikiwa kupata mafanikio ya kazi zao za sanaa ili waweze kufaidi matunda ya nguvu kazi zao.

Nahreel ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na kipindi cha UJENZI kinachorushwa na EATV wakati akielezea namna kazi za sanaa zilivyowawezesha yeye na mpenzi wake Aika kuanza ujenzi wa nyumba yao itakayogharimu shilingi milioni 700.

''Wasanii wanapaswa kujua kwamba muziki unalipa na wakati mwingine haulipi hivyo pale pesa zinapopatikana zitumike katika kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatasaidia wakati wote'' Amesema Nahreel.

“Tumechoka kukaa kwenye nyumba za kupanga tukaamua tutumie tulivyovipata kujenga nyumba yetu ambayo itagharimu milioni 700 ambapo itakuwa ni nyumba ya kisasa na itakuwa na bar ndani yake” amesema Nahreel

Aidha msanii huyo ameongeza kuwa nyumba hiyo itakuwa na ubunifu wa aina yake ikiwemo hata namna ya ufungaji wa umeme, 'sockets' zote zitapita chini tofauti na ilivyo katika nyumba nyingi za sasa.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment

Other news