TANZANIA: Nimeamua kuachia ngoma kwa sababu raia wanamuhitaji Nature – Juma Nature

 

 

 

Msanii ambaye ni moja kati ya watu waliofanikiwa kuitoa bongo fleva shimoni na kuifikisha hapa, Juma Kassim nature, ametoa sababu inayomfanya yeye kuendelea kutoa kazi mpya licha ya ukongwe wake.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Juma Nature amesema ameona mashabiki wake wanakosa baadhi ya vitu kwenye muziki, hivyo amemamua kuja kuwapa ladha nzuri na kuwaonyesha watu ni jinsi gani muziki mzuri unatungwa, na sio kuendelea kutafuta jina kama wengi wanavyodhani.

"Nimeamua kuachia ngoma kwa sababu raia wanamtaka Kibla tena, wanamuhitaji Nature, so kila sehemu ninayoenda kila ngoma wanayosikiliza wanaona kuna mapungufu wanataka nirudi, mi sasa hivi siwezi kuanza kutafuta jina, mi sio underground, nimekuja kutoa ngoma kwa ajili ya mashabiki na wajue muziki bora unatungwa vipi", alisema Juma Nature.

Juma Nature ambaye kwa sasa ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la 'Mtumba', amesema ameamua kuupa jina hilo wimbo wake, kwani mara nyingi muziki wake unakaa muda mrefu bila kuisha mapema kama nguo ya mtumba ilivyo, na asili ya muziki uliopo sasa hivi kwenye game ya Bongo fleva

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment

Other news