TANZANIA: Mfumo wa elimu uliopo unachangia wanafunzi kutopenda shule – Sauti Sol

 

 

Kundi la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol, wamezitaka serikali za Afrika Mashariki kuboresha mifumo ya elimu katika nchi zao, ili kuweza kusaidia vijana kupenda wanachokifanya.

Sauti Sol wamesema mfumo wa elimu uliopo unachangia wanafunzi kutopenda shule na kufanya matukio mabaya kama kuchoma moto shule, kwani sio rafiki kwao.

“System ya education ambayo tuko nayo haijachukua muda kuelewa wanafunzi, so ningependa ichukue time as a system ielewe watoto wa siku hizi walivyo, homework imeongezwa, time imeongezwa, holiday imefupishwa na katika holiday pia lazima uende shule usome, tumetilia mkazo sana katika mitihani, tumesahau kuwa elimu si mitihani”, alisikika mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo.

Sauti Sol waliendelea kusema kuwa umefika wakati nchi za Afrika Mashariki kubadili mfumo wa elimu uliopo, kwani wa sasa umebagua baadhi ya masomo ikiwemo yale ya sanaa, na kutoyapa kipaumbele, hivyo kufanya sio kazi za kuaminika kwenye jamii.

“Hii pia ni motisha kwa serikalii, education yetu system yetu lazima irekebishwe kiasi, unajaza fomu za kuingia university unaona kuna bio chemistry, physics, journalism, huoni hata music, labda wewe talanta yako ni kuchora, especialy East Africa government, kuwa mtu wa maana katika society lazima uwe injinia, daktari, serikali it self imeelevate some careers peke yake, so any student ambaye anapitia katika hiyo system anafikiria kuwa daktari au injinia”, walisema Sauti Sol.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment