a FALLEN ANGEL rylics

yoh!!
wanasema nilipenda bila tija / sikutaka kujifunza sikutaka tiba/ nilikupenda na mtaani ilikuwa shida/ nikakosana na watu maana nilikutaja kila mida /

nikagombana na wana uliposema nipunguze marafiki/ ulihisi wengi wao wanafiki / ukasema niache mziki / nikaacha nikatafuta kazi ilimradi nipambane na dhiki /

na mimi nikaona shega/ kama kuna boya yeyote atanilaumu yamkini bado hajapenda/ niliitika uliponita nilifika nikakusikiliza/ kila uliponituma nilikwenda/

na kama kupenda ndio ajabu /, nimekonda nakupenda ndio sababu /mi kufanya maamuzi si jasiri /kwa sababu yako wala sikujiuliza mara mbili / ah!

kisa wewe nikabuni kila mishe/Nikapigana mpaka na kikundi nikuridhishe/ nilikuwa mwoga nielewe/ kuwa chochote kinawezekana kisa wewe/

niliamua nikupende bila doubt /nikasimama kila nilipoulizwa nikashout/ sikuogopa ugonjwa wala mauti/ kwa sababu yako nikakamatwa boda Sauzi /

nikukumbushe shule nilikuwa King kwenye dorm fights / ila nikapigwa na jamaa kwenye prom fight/ mahusiano yetu yalinicost/ kuna kipindi nilikosa dili nikazama mgodi/

naumwa mama hizi shida zipo/ mama yako alipata ajali nikatoa figo/ nina mafua nakuhitaji kama chafya/ ili nitoe nakupenda mpaka unanigharimu afya/

napenda hip hop lakini nikajua reggae/ sikuwa tozi lakini nikajua chepe/ nikazijua tembe /kichwa kilipokuuma/ nikazama kutafuta ni mapenzi sikuwa bwege/

nikijitosa kuwa usafiri nikufikishe / niliamua kuwa hata mwizi nikuridhishe/ kaka zako walipanga dili/ ili waniue wakaishia kuniumiza nikakanda mwili /

nilikupenda peke yako sikujua mingo/ kuna kipindi uliniweka kwenye matatizo/ kwenye vikoba ulikopa hela mpaka/ nikakamatwa mimi nikafungwa jela mwaka/

sikukoma sio kwamba nilitaka kufa na mali/ sikutaka uteseke nikakupa nyumba na gari/ dili zikabuma tarehe za kulipa zikatimia/ wadeni wakaja nikakimbia/

nilipambana sana nikakosa dili/nikasafiri nikaenda kwa mganga niwe tajiri/ sikupenda mwenzangu ufuturu njugu/ nikavuka ukuta mpaka nikaanza kumkufuru Mungu/

ndugu walinikimbi nakili/ walihisi zimenikimbia akili/ walidhani simple kuniasa/ walifikia kusema nakupenda wewe kuliko maza/

nikavunja miiko/ mpaka nikabadili dini nikawa Mkristo/ nilihadaa kufa/ tulikosa mboga nikagaa gaa na upwa/

ulipenda kupendeza / kugeza mitindo ulipenda kuongea kiingereza/ nikakulipia shule ulifanya madudu/ nikakubali ili usome mimi nibakj mbumbumbu/

nilipigana kila shari ilipokuja nilizuga, mi ni mwalimu kwa baba'ako/ nikafulia wakaniita McMugga, na mtaani nikawa adimu kwa ajili yako/

nilitaka uwe mke ni habari/ nilitamani nikupeleke nje ya sayari/ kuna muda nilisanda nikazama kila chaka sikuogopa nge ni hatari/

kwa yangu hiyari nikawa pusha/ nikajifanya dalali nikauza gari na nyumba/ mentali sikungoja zali kunikuta/ mali ulipofuja zote nikaenda mbali kutafuta/

ulitamani rasta nikasuka/ ulitamani shamba na duka/ ulitamani khanga nikakupa/ sikuogopa nikakudaka ulipoanguka/

washikaji walisema naoa lawama/ nikafunga vioo tukafunga ndoa ya gharama/ kazini nikabeba pesa kwakuwa nilikuwa cashier/ nikakata tiketi twende honeymoon Philadelphia/

sikukwambia haya yote tangu mwanzo/ sikupenda uteseke na mawazo/ nilikulea ka baba'ako/ sio mimi yalikuwa ni mapenzi juu yako/

nilishiriki magendo/ mpaka kuua, nilitaka kuwa mjeda nikashiriki depo/ nilitamani kukuoa kiukweli ndio maana muda wote huo hatukushiriki tendo/

sikuibuka kilingeni/ nikafunga decoder na subwoofer sebuleni/ kuna kipindi nilikumbwa madeni ili upate saluni, nikajenga nyumba ufukweni/ aisee

nitapunguza vipi machungu? /nilikosa kosa kipi kwa mungu/ umekufa sikuoni tena getoni/ umeniacha mola akulaze pema peponi (amen)

Leave your comment