TANZANIA: Msami anasema hana tatizo lolote na Quick Rocka

 

 

 

Kale kamchezo ka kunyakuliana ambako kalikuwa kametawala kwa mastaa wa kike bongo sasa kamehamia kwa mastaa wa kiume pia. Baada ya Msami kuamua kumrukia bi dada Kajala ambaye ni bebe wa Quick Rocka.

Hata hivyo Msami alisema Kajala ni mtu wake wa karibu saana japo watu wanahisi kuwa wao ni wapenzi lakini sio mbaya kwa kuwa Kajala ni mtoto wa kike na yeye ni mwanaume kwa hiyo yeye haoni hatari hata ikiwa hivyo.

 

 

Hata hivyo Msami anasema hana tatizo lolote na Quik na wala hawajanyanganyana ma babe kama watu wanavyoongea na kwamba yeye alivyoshuka kwenye gari lake hakumuona Quick hivyo watu wasimnukuu vibaya kuwa ana bifu na yeye.

Msami amesema kama ikitokea anapendana na Kajala atajua tu kuwa atasimamaje pale mume wa Kajala ambaye anatumikia kifungo jela na kusema yeye ni mwanaume hivyo atajua anamega kisela au wanamwagana.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news