TANZANIA: Nuruelly kwa uwezo aliokuwa nao kwenye muziki alikuwa anastahili kuwa na tuzo nyingi - Nikki Mbishi

 

 

Rapa Nikki Mbishi amefunguka na kusema kuwa msanii kama Nuruelly kwa uwezo aliokuwa nao kwenye muziki alikuwa anastahili kuwa na tuzo nyingi kuliko wasanii wa sasa ambao wanajisifu kuwa na tuzo nyingi.

Nikki Mbishi alisema hayo kupiti kipindi cha eNEWS na kusema anashangaa kuona vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kuwapa support wasanii ambao hawana uwezo kisanii na kuuwa vipaji vya ukweli kwa kutowapa support katika kazi zao.

 

 

"Unajua vyombo vya habari vimekuwa vikitoa nguvu kubwa kwa wasanii wasio na uwezo jambo ambalo linapelekea kuwauwa kisanaa wasanii wenye uwezo wao, leo hii msanii kama Nuruelly alitakiwa kuwa na tuzo nyingi mpaka kabati ivunjike kutokana na uwezo wake wa kuimba lakini ndiyo hivyo tena, huyu alitakiwa kuwa na tuzo nyingi kuliko hata hawa makorokocho wanaojisifu na tuzo, sihitaji kuwataja majina lakini wanajijua wenyewe" alisema Nikki Mbishi

Mbali na hilo Nikki Mbishi alidai kuwa kwa sasa wasanii hao ambao hawana uwezo wameua thamani ya muziki wa bongo fleva ndiyo maana hakuna msanii mwenye uwezo wa kujaza watu kwenye show akiwa pekee yake, kama ilivyokuwa zamani msanii mmoja tu alikuwa na uwezo wa kujaza uwanja na kufanya show.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment

Other news