TANZANIA: Tv za Kibongo zinanitosha kabisa huko nje nendeni nyinyi - Rama Dee

 

 

Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya 'Kipenda Roho' Rama Dee amefunguka na kusema kuwa hana mpango ya kuhangaika na kazi yake kuonekana katika vituo vya nje ya nchi kwani yeye anaamini vituo vya televisheni vya nyumbani vinamtosha kuwafikia mashabiki zake.

Rama Dee siku ya Ijumaa aliachia video yake kwenye kipindi cha Friday Night Live na kusema kuwa ameamua wimbo huo kuupa nafasi kubwa kwa kufanya video za aina mbalimbali kutokana na ukubwa wa wimbo huo.

"Tv za Kibongo zinanitosha kabisa huko nendeni nyinyi. Kipenda Roho haitapatikana kwenye tv za huko itapatikana kwenye Tv za hapa Asante, Part two ipo njiani" aliandika Rama Dee. Msanii huyo anategemea kuachia video nyingine ya wimbo huo ambayo imetayarishwa na Adam Juma.

 

Unaweza kutazama hapa video ya wimbo wake wa 'Kipenda roho':

 

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment