TANZANIA: Dully ana mambo ya kitoto - TID

 

Msanii TID amevunja ukimya na kuelezea chanzo cha ugomvi wake na Dully Sykes, ambao umeanza kuwa gumzo kwa mashabiki. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East AFrica Radio, TID amesema Dully Sykes hakupenda kitendo cha Joh Makini kuwepo kwenye collabo yao ya wimbo wa confidence.

"Kwanza ile ngoma mwenyewe ndio alitaka kuwepo baada ya kuisikia, akasema mnyama hii ngoma kali naomba niweke sauti na mimi, nikamkubalia tukarekodi, lakini alivyokuja kusikia Joh Makini yupo akanipigia simu tena usiku, akaanza kunifokea, tena imagine ngoma yangu ananifokea.TID vp unaweka watoto wa Arusha? ndo unafanya nini?" , alisema TID

TID aliendelea kwa kusema kuwa licha ya hilo baada ya kuandaa show ya ku-launch audio, alivyoona na Joh Makini anaperfom, akampigia Joh akimwambia asikubali kufanya show bila kumlipa.

"Baada ya hapo akampigia Joh akamwambia Joh ile show kubwa usikubali kuperfom bila kukupa milioni tatu, baadaye Joh akaniambia kwamba bila mkwanja haparfom, nikamuuliza we habari hizo umezitoa wapi? akaniambia ni Dully kanambia, nikamwambia ungejua huyo Dully alimind kusikia we upo kwenye ngoma! bahati nzuri siku Dully ananipigia kina nNicotrak walisikia", alisema TID.

TID aliendelea kusema kuwa Dully ana mambo ya kitoto hivyo anahitaji kuacha ushindani usiokuwa na faida, na kushindana kikazi

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment